Karibu – Kiswahili – Swahili

Tovuti hii inatoa vitabu kadhaa vya Profesa David Gooding na Profesa John Lennox. Kwa sasa tuna kitabu kimoja katika Kiswahili, na tunatumaini kuwa na vitabu zaidi hivi karibuni.


Ufalme usiotetemeka : mafundisho juu ya barua kwa Waebrania

An Unshakeable Kingdom

Barua kwa Waebrania inatukumbusha maneno makubwa juu ya Bwana wetu Yesu Kristo - uungu wake, umutu wake, ufufuko wake toka wafu, kwenda kwake mbinguni, na ya kwamba atarudi tena. Lakini kuna maonyo mengi vilevile ndani ya barua hii. Mbele ya kuanza kusoma na kueleza barua hii tuone kwanza kama iliandikwa kwa watu gani, kwa wakati gani, na kwa sababu gani. Kujua maneno haya kutatusaidia kufahamu nini Mungu anataka kutufundisha sisi kwa njia ya barua hii, na roho zetu zitafurahishwa na maneno ya ajabu tutakayosoma juu ya Bwana wetu Yesu Kristo. Kutatusaidia vilevile kupokea maonyo ya barua hii kwa sisi wenyewe na kuyanyenyekea. Haifai tujifurahishe na maneno matamu tu tunayoyasoma ndani ya Biblia bila kuwaza na kunyenyekea maonyo yanayoandikwa ndani yake kwa sisi. Tukumbuke ya kwamba barua kwa Waebrania ni sehemu ya Neno la Mungu lisiloweza kugeuka kamwe.


David W. Gooding (1925-2019) alikuwa Profesa Aliyestaafu wa Agano la Kale la Kigiriki  katika Queen’s University Belfast na Mwanachama wa Chuo cha Royal Irish Academy. Alifundisha Biblia kimataifa na kutoa hotuba mihadharani juu ya uhalisi wake na umuhimu kwa falsafa, dini za ulimwengu na maisha ya kila siku. Alichapisha kazi za kitaaluma na maarufu, ambazo zimechapishwa katika lugha nyingi.


This website makes available a number of books by Professor David Gooding and Professor John Lennox. At present you can download one book in Swahili, and we hope to provide more soon.

Jisajili na anwani yako ya barua pepe ili kupokea habari na masasisho.

Tutumie barua pepe na tutakujibu haraka iwezekanavyo.